Meja Kunta afichua kilichomsukuma afanye ngoma na Chidi Benz

Meja Kunta afichua kilichomsukuma afanye ngoma na Chidi Benz

Mwanamuziki wa Singeli, Meja Kunta, ameweka wazi mipango yake ya kufanya kazi na rapa mkongwe Rashidi Abdallah, maarufu kama Chidi Benz.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanachi Scoop leo,Julai 10, Meja Kunta alifichua kuwa ushirikiano na Chidi Benz umekuwa ndoto yake ya muda mrefu.

" Kwanza kabisa kati ya wasanii wakongwe ambao ninawakubali ni Chidi kabla hata sjaanza kuimba singeli na nilitamani siku moja nije kufanya naye kazi ya pamoja na hatimaye imekuwa kwa sababu ni msanii ambaye anajua nini anatakiwa kufanya katika masuala ya muziki,” amesema Meja Kunta.

Anaamini kuwa ngoma watakayoshirikiana itakuwa na mapokeo makubwa na mazuri kwa mashabiki wa muziki wa Singeli.

“Ujio wa wimbo huo utakuwa kama singeli michano naamini itakuwa na mapokeo mazuri na makubwa kwa watu kwa sababu Chidi ni mkubwa kuliko watu wanavyofikiria kwa sababu mtu akipata wasaa wa kusikiliza namna alivyochana kwenye huo wimbo ni hatari sana” amesema Meja.

Meja pia alifunguka kuhusu urahisi wa kufanya kazi na Chidi Benz, akielezea kuwa upendo na heshima kati yao umesaidia kuimarisha ushirikiano wao.

“ Unajua Chidi ananipenda mimi pamoja na ngoma zangu nakumbuka aliwahi kunitafuta na kuniuliza kuhusu wimbo wa ‘Hassani’ kama nimefanya kwa sababu mara ya kwanza hakuamini so alinisifia sana hapo ndiyo tukatamani kufanya kitu kwa pamoja,” amesema.

Mbali na kufichua mipango ya kazi na Chidi Benz, Meja Kunta alibainisha kuwa anazingatia sana vipaji na aina ya muziki anayotaka kuufanya katika kazi zake.

“Mimi huwa naangalia talent ya mtu na aina ya muziki ambao nataka kufanya kwa muda huo hayo mambo mengine sijui amefanya nini au anatabia gani mimi huwa siyafatilia sana naweka mbele muziki mzuri tu na uwezo wa mtu” amesema

Meja Kunta pia ameongezea kuwa wimbo huo utakuwa tayari kusikilizwa masikioni mwa watu baada ya wiki moja hivyo amewataka mashabiki wa singeli na michano wakae mkao wakula.

Utakumbuka msanii huyo amefanya nyimbo kama, Bado haujasema, Hassani, Tabia mbaya, Ushali, Mamu, Kidimbwi, Demu wangu, Madanya ya mke wangu na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post