Megan haoni sababu ya kupatana na Nicki Minaj

Megan haoni sababu ya kupatana na Nicki Minaj

Rapa wa Marekani Megan Thee Stallion amefunguka kuwa hayupo tayari kupatanishwa na msanii mwenzake Nicki Minaj, kwani hajui chanzo cha ugomvi wao.

“Mpaka leo sijui tatizo ni nini, sijui hata nini kinaweza kutupatanisha kwa sababu mimi, mpaka leo, sijui tatizo ni nini,” amesema Megan

Utakumbuka kuwa ugomvi wa wawili hao ulianza baada ya Megan kuachia wimbo wake wa ‘Hitt’ ambao ulitafasiriwa kama amemtupia dongo mume wa Nicki ‘Keneth Petty’ jambo lililopelekea Nicki arudishe mashambilizi na kumjibu kupitia ngoma ya ‘Big Footy’.

Mbali na hayo bifu lao lilifika pabaya zaidi baada ya mashabiki wa Nicki Minaj waliojulikana kama ‘Barbz’ kuchapisha picha ya sehemu ambayo lipo kaburi la marehemu mama Megan huku wakitishia kwenda kulivunja jambo ambalo lilipelekea polisi kuweka kambi katika eneo la kaburi hilo .

Nicki Minaj na Megan Thee Stallion waliwahi kuwa marafiki wa karibu hadi kufanya ‘kolabo’ mbalimbali ikiwemo ‘Hot Girl Summer’ ya mwaka 2019 na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags