Megan atuhumiwa kwa unyanyasaji wa kihisia

Megan atuhumiwa kwa unyanyasaji wa kihisia

Mwanamuziki kutoka Marekani, #MeganTheeSTallion amefunguliwa mashitaka na aliyekuwa mpiga picha wake #EmilioGarcia kwa unyanyasaji wa kihisia na mazingira magumu ya kazi.

Emilio kwenye shitaka hilo amedai kuwa Juni mwaka 2020 Megan alimlazimisha amtazame akiwa anafanya ngono katika gari kisha baada ya tukio hilo alimuonya kuwa asiseme chochote alichoshuhudia ili kulinda heshima ya rapa huyo.

Hata hivyo kwa upande wa Megani mwenye umri wa miaka 29 bado hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili.

Ikimbukwe kuwa mwaka jana mwanamuziki huyo alimshitaki #ToryLanez kwa kumpiga risasi mguuni mwaka 2020 ambapo mpaka sasa rapa huyo anatumikia kifungo cha miaka 10 gerezani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags