Duniani kumekuwa na michezo ya aina nyingi sana ambayo yote huwa na mashabiki wake ambao mara nyingi wanakuwa na mapenzi ya dhati kwa timu zao hadi kufikia hatua ya kufanya chochote kwa ajili ya timu hizo pale zikifungwa ama kufunga.
Mara nyingi mashabiki huwaza matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji wao na ndiyo maana ikitokea wakapoteza katika mchezo mashabiki hutokwa na maneno mengi ya kujitetea.
Katika mchezo wa mpira wa miguu kama unadhani si jambo rahisi kwa timu moja kumfunga mpinzani wake goli 20 au zaidi ndani ya dakika 90 basi tambua kuwa mwaka 1950 timu ya Taifa India ilimchapa Nigeria goli 99-1.
Inaelezwa kuwa mwaka 1950 timu ya India ilifanikiwa kumchapa Nigeria goli 99 kwa moja kwenye FIFA World Cup, ambapo mara zote India ilikuwa ikishika mpira basi inatia nyavuni, katika mchezo huo.
Baada ya kichapo kukolea kwa Nigeria ndipo mchezaji mmoja aliyeitwa Samuel Okwaraji akajitoa muhanga na kufanikiwa kuingiza goli moja la kufutia machozi ambalo liliwafanya mashabiki wa Nigeria kuamka kwa shangwe wakishangilia goli hilo.
Kichapo hicho kilizua gumzo miaka hiyo na ndipo wachezaji kutoka Nigeria walidai kuwa kila walipokuwa wakipiga mpira uligeuka na kuwa simba, huku mchezaji huyo aliyefanikiwa kufunga goli ndiye alidai kwa upande wake aliuona mpira ukigeuka na kuwa jiwe, hivyo walipatwa na hofu iliyofanya wafungwe magoli mengi kiasi hicho.
Kutokana na tuhuma hizo FIFA iliweza kuifungia India kucheza mpira wa miguu, kwa kosa la kugoma kuvaa viatu wakati wa kucheza mchezo huo uwanjani na kwa kutumia mbinu zisizofaa katika mechi hiyo.
Leave a Reply