Mchoro wa picha ya marehemu Kobe wamponza mmiliki wa gym

Mchoro wa picha ya marehemu Kobe wamponza mmiliki wa gym

Mmiliki wa gym ya Hardcore Fitness iliyoko jijini Los Angeles ajikuta kwenye vita na mwenyenyumba, baada ya kuweka mchoro wa marehemu Kobe Bryant na wanaye katika ukuta wa nyumba hiyo aliyopanga kwa ajili ya kutolea huduma za mazoezi.

Mwenyenyumba huyo aonekana kukasirishwa na mmiliki wa gym hiyo ayefahamika kama Cecilia Moran baada ya kuweka mchoro wa Kobe na mwanaye kama kumbukumbu ya mchezaji huyo wa mpira wa kikapu ambaye alifariki kwa ajali ya ndege Januari 26, 2020.

Cecilia ametakiwa kuondoa mchoro huo mwishoni mwa mwezi huu, lakini kwa upande wake ameonekana kutokuwa tayari na amri hiyo ya mwenyenyumba wake.

Akiwa anazungumza na vyombo ya habari Cecilia amedai kuwa amepokea notisi ya mwezi mmoja kuwa ni lazima aondoe mchoro huo wa kumuenzi marehemu Kobe na mwanaye wa kike, hata hivyo Cecilia amedai kuwa mchoro huo umekuwa chachu kwa wanamazoezi na mashabiki wa Lakers hivyo basi mwenyenyuma afikiri upya na ikiwezekana amtoze ushuru wa kulipia picha hiyo.

Hivyo basi Cecilia ameomba wananchi kuingilia kati swala hilo kumsihi mwenyenyumba kumpa ruhusa ya kuwa na mchoro huo katika ukumbi huo wa kufanyia mazoezi.

Ikumbukwe Kobe alikuwa ni mchezaji wa mpira wa kikapu Los Angeles Laker katika National Basketball Association (NBA) alifariki dunia kwenye ajali ya ndege akiwa na mwanaye wa kike aitwaye Gianna na watu wengine saba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags