Mchezaji Victor kuichukulia hatua ‘klabu’ ya Napoli kwa kumdhihaki

Mchezaji Victor kuichukulia hatua ‘klabu’ ya Napoli kwa kumdhihaki

Mchezaji wa ‘timu’ ya taifa nchini Nigeria, Victor Osimhen, inadaiwa anampango wa kuchukua hatua za kisheria kutokana na ‘klabu’ ya #Napoli, kumdhihaki kwa kutumia video yake inayosambaa kwenye mtandao wa TikTok ambayo ‘klabu’ hiyo ime-share kwenye mtandao huo.

Video hiyo ilimuonesha Victor akikosa mkwaju wa ‘penati’ katika ‘mechi’ yao dhidi ya ‘klabu’ ya #Bologna siku ya Jumapili, na kumalizika kwa matokeo ya sare.

Kisha video nyingine ilikuwa na maneno “I’M A COCONUT” yakisikika, ambapo mchezaji huyo ametafsiri kama dhihaka juu yake.

Hata hivyo wakala wa mshambuliaji huyo, #RobertoCalenda alithibitisha kuwa walichofanya ‘klabu’ hiyo dhidi ya mteja wake hakikubaliki, na kwamba mchezaji huyo ana haki ya kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.

Kwa sasa hiyo video imeondolewa kwenye mtandao wa TikTok na ikumbukwe kuwa Osimhen aliwahi kuisaidia ‘timu’ hiyo kuwa miamba wa ‘soka’ nchini Italy.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags