Mchezaji wa ‘timu’ ya taifa ya Brazil Richarlison ameweka wazi kuwa kwa sasa anahitaji msaada wa ‘kisaikolojia’ atakaporudi England baada ya kupitia changamoto nyingi katika maisha yake ya ‘soka’.
Msaada huo anahitaji baada ya mchezaji huyo wa ‘klabu’ ya Tottenham kucheza ‘mechi’ nne za mwisho za Brazil bila ya kufunga mabao jambo ambalo limempatia wakati mgumu, hivyo anataka msaada wa ‘kisaikojilia’ kwani hali hiyo inamtesa sana.
“Nahitaji msaada haraka wa ‘kisaikolojia’ inaniumiza sana, akili yangu inatakiwa kufanya kazi, nikiwa uwanjani najaribu kufurahi na wachezaji wenzangu lakini haisaidii, napambana kwa ajili ya ‘timu’, wakati mwingine mambo hayaendi kama ninavyotarajia.
Nadhani haya mambo yanachangiwa na mambo binafsi yanayotokana na mambo ya nje ya uwanja. Hata kama nataka mambo yangu yaende sawa, mwisho wa siku yanaenda tofauti.”
Richarlison amepitia changamoto hizo ndani ya miezi 12 akiwa Tottenham kwani amefunga mabao manne katika ‘mechi’ 40 alizocheza.
Leave a Reply