Mbinu za kuonekana stylish ofisini

Mbinu za kuonekana stylish ofisini

Eiwaaaah !!!its Friday day bwana kama kawaida karibu kwenye ukurasa wa fashion, sehemu pekee ambayo inakuongoza vyema kabisa kuhusiana na masuala muonekano wako.

Nikuweke bayana kuwa wiki hii aiseee tutakwenda kuangazia namna ya kuonekana Stylish ofisini kwako aloooh sio unajivalia tu bure niende no kata kabisa hiyo roho.

Suala la kuwa stylish unaweza kuhisi na kuogopa ukasema aaaah bwana weee!!! Gharama lakini nikwambie tu kwenye issue ya kuweka muonekano wako achana kabisa na mambo ya kufikiria gharama.\

Leo ngoja nikuelekeza namna gani unaweza kutokelezea tena kwa gharama nafuu kabisaa ukiwa ofisini bwana ungana name kupitia dondoo hii ya fashion tujifunze kwa pamoja.

Nikwambie tu moja kati ya vitu ambavyo wengi tunapitia ma-ofisini ni kuwa confused kati ya kuwa over dress na ku-low dress ofisini na chaguo kubwa kuwa katikati yaani usiwe low wala over dressed.

Hahaha aloooh hapa ndipo tunapokutana wengi unakuwa na ma shirt yako ya rangi moja kadhaa, skirt kadhaa na suruali ukamalizia na handbag yako na viatu basi mwisho wa siku ofisi nzima tunafanana kasoro rangi za nguo tu lakini ni namna gani unaweza kuwa stylish ofisini?

Hili ni swali la kujiuliza na majibu yake ni mepesi bwana wala usiogope na tunaazna kama ifuatavyo mwana mitindo mwenzangu.

Toka Kwenye Plain Clothes Na Anza Kuvaa Pattern

Asilimia kubwa ofisini tunavaa plain clothes utakuta umevaa plain white shirt na plain black trouser au skirt, toka hapo na anza kuvaa zenye pattern kama top plain basi chini valia suruali/skirt ya pattern na kama skirt / suruali plain valia top yenye pattern hakikisha rangi zinaendana 

Vaa Mavazi Ya Rangi

Hakuna sehemu imeandikwa rangi za mavazi ya kazini yawe black, white, au blue tu jamani hahaha nakukumbusha tu  kuna colors nyingi ambazo zina pop lakini zimetulia vyema tu unaweza kuvaa ofisini kama maroon, emerald green, mustard yellow etc lakini pia hakikisha hazipigi kelele sana na kama utavaa juu rangi ina pop chini vaa calm color.

 

Pop Color Na Viatu / Handbag

Ebwana eeeh kama sio mpenzi wa mavazi ya rangi rangi basi kati ya viatu au handbag hakikisha ina rangi ya kuvutia ambayo itafanya wengine wageuze shingo kukuangalia wewe

Accessorize

Hili nalo lakuzingatiwa sana jamani tunapombana kutafuta mionekano bora makazini basi suala la accessorize mfano miwani sio mpaka uwe unaumwa macho jamani .

Nikuelekeze sasa unaweza kuvaa tu kama accessory kuna miwani ambayo ni kama ya macho lakini ni ya urembo unaweza kuchagua unayoona inakufaa ukavaa, vaa belt pale vazi lako ninapohitaji mfano unavaa black little dress unaweza kuongezea na animal print waist belt, pochi pia inaweza kuwa namna nzuri ya kuongezea udambu udambu  kwenye vazi lako la ofisini.

Yap bila shaka umenifahamu vizuri kabisaaa mwanamitindo mwenzangu wewe sasa kuamua namna utakavyotaka uonekani ukiwa ofisini kwako jichagulie muonekano bwana happy wikiend epuka kuwa hovyo ofisini.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags