Mbasha adaiwa kuchomwa kisu na mtu asiyejulikana

Mbasha adaiwa kuchomwa kisu na mtu asiyejulikana

Inadaiwa msanii wa nyimbo za injili nchini, Emmanuel Mbasha yupo hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam kwa matibabu baada ya kuvamiwa na kuchomwa visu kifuani na mtu asiyejulikana.

Mdogo wa msanii huyo Onesmo Mbasha ameeleza jinsi alivyovamiwa mwanamuziki huyo anasema kuwa kaka yake alipatwa na tukio hilo akiwa barabarani baada ya kugongwa na gari iliokuwa inamkimbiza ndipo alisimama na kwenda kumuulza mtu aliyemgonga kisha akaanza kushambuliwa na kisu kifuani na mbavuni.

Ingawa mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi ya utambuzi wa mtu aliyefanya tukio hilo, Mbasha bado yuko hospitali anapatiwa matibabu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags