Mawakili wa Diddy waipangua kesi moja

Mawakili wa Diddy waipangua kesi moja

Mawakili wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani #PDiddy ambaye anakabiliwa na kesi mbalimbali za unyanyasaji wa kijinsia wamesema wana mpango wa kuyakataa madai ya moja ya kesi  za mteja wao kwasababu yamedaiwa kufanyika kabla ya sheria mpya anayotuhumiwa nayo kuivunja haijatungwa.

Kulingana na tovuti ya TMZ New imeeleza kuwa hati mpya iliyopatikana inasema kuwa mawakili wa Diddy wamejibu tuhuma zilizotolewa na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Joi Dickerson ambapo Novemba mwaka jana alifungua kesi akidai kuwa alinyweshwa dawa za kulevya na kunyanyaswa kingono  na Diddy mwaka 1991.

Pamoja na Joi kuwasilisha tuhuma zake, lakini mawakili wa msanii huyo wamedai kuwa mteja wao hawezi kushitakiwa kwa madai kadhaa kati ya hayo kwa sababu kuna sheria hazikuwepo wakati wa miaka hiyo.

Diddy yupo katika hali mbaya ya kukabiliwa na kesi hizo ambapo Machi 26, 2024 Jeshi la Polisi nchini humo walipitisha msako katika nyumba yake kama sehemu ya uchunguzi wa Serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono na madawa ya kulevya yanayo muhusisha msanii huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags