Mavazi yanayo pendelewa kuvaliwa msimu huu wa mvua

Mavazi yanayo pendelewa kuvaliwa msimu huu wa mvua

It’s furahidayyy!! wanangu sana kama kawaida sisi nia na madhumuni yetu ni kukupasha yale yote unayo yasikia, naunayo yajua kwa uchache basi kwetu katika uwanja wa fashioni tunakujuza zaidi.

Leo katika fashion nimekusogezea mavazi yanayo stahiki kuvaliwa hasa katika kipindi cha mvua, kama tunavyojua ifikapo miezi ya Machi, Aprili na Mei maeneo mbalimbali nchini hupata mvua za masika.

Katika kipindi hicho cha mvua baadhi ya watu hupata changamoto katika kuchagua mavazi haswa katika maeneo ambayo mara nyingi hupata vipindi vya joto kwa mwaka.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya mitindo ya mavazi wanashauri kuwa ni vyema kila mtu kuhakikisha katika kabati lake ana mavazi ya aina mbalimbali ambayo anaweza kuvaa katika misimu yote iliyopo katika mwaka hii inapendeza zaidi mtu akavaa vazi kutokana na majira.

Mfano inapofika kipindi cha mvua, kiangazi, masika au vuli basi ni vyema kujiandaa kwa kua na nguo ambazo msimu husika ukifika basi unaweza kuvaa.

Basi bwana team ya Mwananchi Scoop ikaendelea kufuatilia ukweli wa mambo ndipo tukapata wasaa wa kuzungumza na bwana Abdallah Shabani makazi wa Chanika jijini Dar es salaam yeye alisema kuwa inapofikia nyakati za mvua huwa ana hakikisha masweta au makoti havikosekani katika kabati lake.

Hatukukata tamaa tukaendelea na safari mpaka tulipofika Goba tukakutana na Amina Salum mkazi wa Goba anasema kwa upande wake inapofikia nyakati za mvua nyingi anahakikisha hakosi mwamvuli pamoja na buti kwaajili ya kujikinga na mvua anapotoka kwenda kwenye shughuli zake

“Pia huwa napendelea kuvaa nguo nzito bila kusahau soksi miguuni ili kujikinga kama mvua hiyo itaambatana na baridi kali”anasema Amina.

Akizungumza na Mwananchi Scoop mbunifu wa mavazi Rose Robert kutoka ‘Rosee House of Stylish’ anasema kuwa katika kipindi cha mvua au baridi kali mavazi kama sweta koti, poncho, blazer, pullneck havitakiwi kukosa katika kabati la mtu anayependelea kuvaa kulingana na wakati.

Pia viatu ambavyo havipitishi maji kama vile buti, snika na vinginevyo na hata vikipitisha basi viwe vinakauka kwa haraka kama vile 'open shoes.

Rose anasema kwa wale wanaopendelea kuvaa nguo fupi katika kipindi hiki inapendeza zaidi uvae na koti refu na buti refu kwenda juu ili kuzuia baridi miguuni.

“Inapendeza kwa mtu anaevaa nguo ndefu basi atupie koti lenye urefu wa wastani na kwa yule anaevaa nguo fupi basi avae na koti refu “amesema.

Aidha aliongeza kuwa katika kipindi cha mvua inashauriwa mtu kuvaa accessories chache ambazo haziruhusu kuingia maji "waterproof".

Mwanamke na mwanaume katika kipindi hiki anaweza kuvaa suruali ikiambatana na sweta lenye urefu wa wastani lililo katika mtindo wa pull neck akitupia na koti miguuni akimalizia kwa kuvaa snika au aina nyingine za raba.

Anaongezea kuwa katika kipindi cha mvua au baridi kali ni vyema kujiepusha na mavazi ambayo rangi yake inachafuka kwa haraka akitolea mfano rangi nyeupe.

Pia kuepuka kuvaa viatu virefu au vile vyenye asili ya kuteleza ili kujiepusha na kujikwaa au kuteleza kwani katika kipindi hicho baadhi ya maeneo huwa na utelezi.


Hata hivyo ni vema kujiepusha na uvaaji wa sketi au gauni za kumwaga kwani wakati mwingine mvua huweza kuambatana na upepo mkali na kukufanya kushindwa kutembea kwa kuwa huru nguo kupeperuka na upepo hatimae mambo yote hadharani.

Eeeeeeh! Nimatumaini yangu tumesomana, yaani sisi bwana mshindwe wenyewe tuu maana tunaenda na nyakati so katika kipindi hichi cha mvua jitahidi sana kujiweka vile inavyotakiwa ili kuepusha magonjwa ya vikohozi na fangasi katika miguu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags