Mavazi ya Malkia Elizabeth II enzi za uhai wake

Mavazi ya Malkia Elizabeth II enzi za uhai wake

Its weekend karibu sana kwenye ukurasa wa fashion na wiki hii bwana moja kwa moja tutakwenda kuangazia mavazi ambayo alikua akipendelea Malkia Elizabeth wa II.

Bila shaka nikurudishe nyuma kidogo ambapo wiki iliyopita tulipokea taarifa za kifo cha malkia huyo mnamo tarehe 8 september, 2022.


Licha ya kufariki akiwa na umri wa miaka 96, Malkia Elizabeth II wa Uingereza ndiye mkuu wa nchi anayeshikilia rekodi ya dunia kuhudumu muda mrefu zaidi maradakani.

Elizabeth II aliukwaa wadhifa wa malkia akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 1952 baada ya kifo cha baba yake, aliyekuwa mfalme wa taifa hilo George VI.

Hadi anafariki katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alikokuwa anapatiwa matibabu, Elizabeth II ameiongoza Uingereza kwa miongo saba.

Moja kwa moja baada ya kufahamu historia fupi ya Malkia Elizabeth II twende tuikatazame kwa picha mavazi ambayo alikua akivutiwa nayo enzi za uhai wake.

Kama mnavyofahamu bwana wakati binadamu yoyote akiwa kijana huwa kuna mavazi flani flani hivi kila mmoja hupendezwa nayo kulingana na mazingira na namna alivyokuzwa kutoka kwenye familia yake.

Yafuatayo ni mavazi aliyokua akiyapendelea zaidi Malkia Elizabeth II wakati alipokua msichana hadi alipofikia utu uzima.


Bila shaka utakua umeziona fashion mbalimbali ambazo alikua akizivaa Malkia huyo na nikukumbushe tu kuwa Mazishi ya serikali ya Malkia yanatarajiwa kufanyika huko Westminster Abbey, Abbey ni kanisa la kihistoria ambapo wafalme na malkia wa Uingereza wanatawazwa, ikiwa ni pamoja na kutawazwa kwa Malkia mnamo 1953.

Apumzike kwa amani.Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post