Mavazi unayotakiwa kuvaa wakati wa usaili wa kazi/interview

Mavazi unayotakiwa kuvaa wakati wa usaili wa kazi/interview

Na Aisha Lungato

 

Another week, another day tunakutana tena katika jarida letu pendwa na mwendo ni uleule kujuzana mambo mbalimbali kuhusu kazi, na kama mwezi huu nimewakamia vile kuhusu usaili wa kazi.

Siku zote unapoambiwa unaenda katika usaili wa kazi basi ujue na uliweke akilini kuwa unaenda katika jambo kubwa na ndio maana lina mada nyingi mno.

Siku ya kufanya interview au usaili ni siku ambayo unatakiwa kuzingatia zaidi muonekano wako kwa sababu ndiyo unaokueleza kuwa wewe ni nani. Ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua ni mavazi gani unapaswa kuvaa katika usaili wa kazi.

Licha ya kuwa kuna baadhi ya ofisi haziangalii mavazi yako na zipo ofisi zinaangalia mavazi yako ila ni vyema ukajiandaa mapema. Kitu cha muhimu na chakuzingatia ni kuweka vyeti na CV zako katika mpangilio uliyo bora.

1.Kufanya utafiti wa mavazi wanayoyatumia ofisi unayoenda kuomba kazi.

Fanya utafiti na fuatilia kwa umakini na kujua mavazi yanayohitajika katika hiyo kazi, uchunguzi wakounatakiwa ujue viwango wanavyoviangalia katika uvaaji. Hata kama uvaaji wao ni wa kawaida, kwenye usaili usiende kawaida.

 


2.Mavazi

kwa mavazi unayotakiwa kuvaa ni kuhusiana na sketi, shati hufanya uonekane kikazi zaidi, kwa mvulana suruali na shati la mikono mirefu na ‘tai’ haina shida inakufanya uonekane mwenye mvuto.

Usiweke marashi makali au vitu vya thamani mwilini kama saa ya bei ghali, hereni za dhahabu inamfanya mwajiri kuwa na wasiwasi na wewe namna gani atakulipa? kama maisha yako ni ghali kuliko mshahara wako.

Upende au usipende, mwonekano wako unachangia namna ambavyo mwajiri atafanya maamuzi ya kukuajiri. Mtazamo unachangia kutokana na mwonekano wako unaweza kuwa ni mtu ambaye unavigezo vyote kielimu lakini mwonekano wako usipokuwa mzuri utaathiri  maamuzi ya kukuajiri, hivyo unatakiwa kujua namna ya kuvaa kulingana na kazi unayoomba .

Uvaaji wako unatakiwa umuoneshe mwajiri au mtu anayekufanyia usaili kwamba unamaanisha kile unachoomba. Unatakiwa kuwa jasiri na mweledi hutatakiwi kuvaa suti, inategemea kazi gani unaomba ila unatakiwa upendeze.

Usiende na mavazi ya kawaida kama Jeans na Tshirt. Ukienda umevaa kawaida mtu anayekufanyia usaili unamwoshesha kwamba hata kazi unaweza kuichukulia kawaida, unapovaa vizuri unaonyesha kujiheshimu na kuheshimu kazi unayoomba.

3.Vitu vya kuviepuka

Usivae sketi fupi, kujipondoa kupitiliza au viatu virefu sana. Kwenye usaili sio sehemu ya maonyesho ya mavazi au manukato gani unatumia pia usivae nguo zenye rangi kali au za kung’aaa.

Cha kuzingatia ni kuwa hata utakapo pata kazi endelea kuvaa vizuri, onesha mafanikio na uonekane unathamini na kujali kazi hivyo kwa namna unavyovaa. Kama unataka kupandishwa cheo vaa kama mwenye cheo hicho, usidharau umuhimu wa mavazi katika eneo lako la kazi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags