Mauzo ya simu za Iphone yashuka duniani

Mauzo ya simu za Iphone yashuka duniani

Mauzo ya simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple yameshuka duniani kote kwa asilimia 10 katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2024.

Hayo yamebainishwa na utafiti uliofanywa na kampuni hiyo ya mawasiliano, ambao umebaini mahitaji ya wanunuaji yameshuka katika sehemu zote duniani isipokuwa Ulaya.

Utafiti huo pia ulibainisha mapato ya kampuni hiyo yalipungua kwa asilimia nne hadi Dola za Marekani 90.8 bilioni ambalo ni anguko kubwa zaidi kuwahi kutokea ndani ya mwaka mmoja. Hata hivyo, bei ya hisa zake katika Soko la Hisa la New York zimeendelea kupanda.

Utafiti huo umesema chanzo cha kushuka ni pamoja usumbufu wa usafirishaji wa bidhaa hizo uliotokea kutokana na sababu zinazohusiana na Uviko-19.

Hata hivyo, Apple imeahidi mauzo yake tena katika miezi inayokuja, ikibainisha uwekezaji zaidi katika Akili Bandia (AI).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya Apple, Tim Cook amewahakikishia wawekezaji kuwa mauzo yataongezeka, ameyasema hayo wakati akizungumzia kushuka kwa asilimia nane kwenye soko la China pekee.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags