Matatizo ya misuli yamtesa Celine Dion

Matatizo ya misuli yamtesa Celine Dion

Dada wa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Celine Dion, Claudette Dion ametoa taarifa mpya kuhusiana maendeleo ya mwanamuziki huyo kwa kuweka wazi kuwa kwa sasa Celine anasumbuliwa na matatizo ya misuli.

Claudette ameeleza kuwa kufuatiwa na tatizo hilo la misuli limemsababishia Celine kupata maumivu huku akiweka wazi kuwa itachukua muda kwa nyota huyo kurejea tena jukwaani.

Licha ya mwanamuziki huyo kuendelea kuandamwa na matatizo lakini Claudette amesema Celine bado ana malengo ya kurejea tena jukwaa.

Ikumbukwe kuwa Celine Dion aliweka wazi ungonjwa unaomsumbua wa ‘Stiff-Person Syndrome’ Disemba 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram na kulazimika ku-cancel matamsha yote aliyopanga kuyafanya mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags