Master J achukizwa wasanii wa bongo kujilinganisha na mastaa wa nje

Master J achukizwa wasanii wa bongo kujilinganisha na mastaa wa nje

Ebanaee!! Imekaaje hii swala la kuiga au kujilinganisha na kila kitu kinachotoka njee ya nchi hususani wasanii wa kibongo kujilinganisha miondoko yao na mastaa kutoka Nigeria or South Afrika wakiamiini kufanya hivyo ndio wanatoba.

Basi bwana mtayarishaji mkongwe wa muziki kutoka MJ Records, Joachim Marunda Kimaryo maarufu kama Master J ameeleza kuhusiana na kutokupendezwa na wanamuziki wanavyo jilinganisha na nchi za West Africa kimuziki huku akitabiria makubwa muziki wa bongo fleva miaka 20 ijayo.

Ameyasema hayo katika mahojiano yake na moja ya chombo cha habari kuwa wanamuziki wa kibongo wanauwezo wakufanya mambo makubwa kuliko kuiga kila kitu kutoka nje.

“Hatuwezi kujilinganisha na nchi ambazo tayari zimeendelea kimuziki wakati sisi bado tunaendelea kujitafuta kwasababu wenzetu wamewekeza pakubwa kwenye mambo mbalimbali husasani kwenye muziki mfano soko la muziki Amerika huwezi kulifananisha na soko jengine”alisema Master J.

Sambamba na hayo ameipongeza tasinia ya muziki kwanzia wasanii, producers na mameneja kuwa miaka 20 ijayo yatatokea mambo makubwa katika mziki wa bongo fleva.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post