Mastaa Watoa Salamu Za Pole Kariakoo

Mastaa Watoa Salamu Za Pole Kariakoo

Kufuatia na tukio lililotokea mapema leo la kuporomoka kwa moja ya jengo Kariakoo na kusababisha maafa pamoja na majeruhi baadhi ya mastaa wametoa salamu zao pole kwa wafanyabiashara na majeruhi.

Kupitia kurasa za Instagram za baadhi ya mastaa wametoa pole kwa kuandika jumbe mbalimbali akiwemo Zuchu, D Voice, Lulu, Idris Sultan, Lavalava, Hamisa Mobeto, Hemed Phd huku wengi wao wakishindwa kutoa ujumbe wowote zaidi ya kuwaombea majeruhi.

“Leo ilikuwa nikumbukizi nzuri ya kusheherekea mwaka 1 toka nijiunge na @wcb_wasafi pamoja na watu wote walio nipokea na wanaoendelea kunisapoti ila imekuwa nisiku mbaya pia poleni ndugu zangu wa Kariakoo,”

“Mungu yu pamoja na nyinyi kwani hakika yeye ni mwenye kusikia tunavyomuomba pongezi pia kwa watu wote na serikali tusiache kuwapambania wenzenu na walio karibu tukazidi kutia nguvu kwa pamoja tutafanikisha hili poleni sanaaa, ila huo ujumbe wa huyo mwana umenifanya nimelia sana”, ameandika D Voice

Kwa upande wa mwanamuziki anayetamba na ngoma ya ‘Nimechoka’ Zuchu naye ameyatoa ya moyoni kwa kuandika.

“Natoa pole kwa ndugu zangu wa K/koo Mungu awape nguvu kwenye kipindi hiki kigumu”, ameandika Zuchu

Naye Idris Sultan amenadika “Pole sana sana na Mwenyezi Mungu akurejeshee moyo wenye nguvu na afya zaidi kwa janga la Kkoo, tutumie moyo zaidi ya akili kuhakikisha tunafanya juu kuokoa watu, asanteni wote mlioweza kushiriki pale wengine tuliposhindwa kusaidia kwenye hili kulizungumza napo iwe nguvu mojawapo kuhakikisha halitokei tena”,

“Hukuna kiwango cha pole kitakachotosha kuwafariji wahanga wa kilichotokea leo Kariakoo, safari yao ya utafutaji imekubwa na changamoto ambayo hawakuiona wala kuitarajia walipoamka asubuhi ya leo”,

“Pole nyingi ziende kwa wafanyabiashara na kila mmoja aliyeathiriwa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Mwenyez Mungu azidi kuwapa nguvu, subira na moyo wa kutokata tamaa kwenye shughuli zao za utafutaji”, ameandika Hamisa Mobetto






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags