Mastaa watatoka vipi leo, Met Gala 2025!

Mastaa watatoka vipi leo, Met Gala 2025!

Zimesalia saa chache, dunia kushuhudia tukio kubwa la mitindo  'Met Gala' linalotarajiwa kufanyika leo Mei 5, 2025 katika jumba la makumbusho Metropolitan Museum of Art, New York Marekani.

Met Gala ni tukio la kiburudani linalohusisha Mitindo na Fashion kutoka kwa watu maarufu duniani, ambao ni pamoja na Waigizaji, Wanamichezo, Mastaa wa Muziki, Matajiri, Viongozi wa Kisiasa na watu wengine wengi.

Tukio hili hufanyika kila mwaka siku ya Jumatatu ya kwanza ya mwezi Mei. Lengo kuu la Met Gala likiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi ya sanaa ya Metropolitan Museum of Art, hasa kwa ajili ya makumbusho ya sanaa ya vitu vya mitindo.

Kauli mbiu ya Met Gala kwa mwaka 2025 inasema ' Superfine: Tailoring Black Style' ambayo imetokana kitabu cha Monica L Miller's, Slaves to Fashion.

Met Gala 2025 ipo chini ya mchezaji wa mpira wa kikapu tokea nchini Marekani, LeBron James, akishirikiana viongozi wasaidizi ambao ni nyota wakubwa kwenye tasnia ya fashion na mitindo. Akiwemo Pharrell Williams, mtayarishaji maarufu wa muziki na mkurugenzi wa ubunifu wa Louis Vuitton Lewis. Huku Louis Vuitton wakiwa ndiyo wadhamini wa Met Gala 2025

Wengine ni mwigizaji Colman Domingo, Asap Rock ambaye ni rapa, mwigizaji, mjasiriamali lakini pia ni mkurugenzi mbunifu wa kwanza kabisa wa kampuni ya miwani ya Ray-Ban aliteuliwa kushika wadhifa huo Februari 2025.

Kiingilio cha Met Gala 2025 ni dola 75,000 sawa na Sh202 milioni ambapo mara nyingi kampuni hununua meza nzima mfano, chapa ya mitindo inaweza nunua meza na kualika watu mashuhuri wanaowataka wao. 

Wageni wanatarajiwa kuanza kupita kwenye zulia jekundu 'red carpet' kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki sawa na saa 6:00 jioni kwa saa za New York.

Mastaa kibao wakitarajiwa kuhudhuria katika tukio hilo kubwa la mitindo siku ya leo ikiwa ni pamoja na Doechii, Usher, Card B, Zendaya, Beyonce, Doja Cat, Kim Kardashian, Rihanna na wengine wengi.

Met Gala ilianzishwa mnamo 1948 na mtangazaji wa mitindo na fashion, Eleanor Lambert ambapo ilifanyika katika tukio la chakula cha usiku na tiketi ya kiingilio iliuzwa kwa dola 50. 

Lakini kuanzia Machi 21,1973 ilianza kufanyika rasmi ikiwa imebeba dhamira ya 'The World Of Balenciaga' huku ikiwa chini ya udhamini wa serikali ya Hispania na tiketi zake ziliuzwa kwa dola 85.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags