Mastaa wa soka wanaoongoza kwa wafuasi Instagram

Mastaa wa soka wanaoongoza kwa wafuasi Instagram

Baada ya kuachiwa kwa orodha ya wanasoka wanaolipwa zaidi, fahamu kuwa wapo nyota wengine wa michezo ambao wanaogoza kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram.

Orodha hiyo inaongozwa na Cristiano Ronaldo, nyota wa soka wa Ureno, ambaye anawafuasi milioni 630, akifuatiwa na mpinzani wake wa muda mrefu Lionel Messi mwenye milioni 503.

Nafasi ya tatu ikichukuliwa na mcheza kriketi kutoka India Virat Kohli akiwa na wafuasi milioni 269, akifuatiwa na nyota wa Brazil Neymar mwenye wafuasi milioni 221 huku nafasi ya mwisho ikienda kwa mcheza kikapu maarufu Marekani Lebron James akiwa na wafuasi milioni 159.

Ikumbukwe kuwa wiki chache zilizopita jarida la Forbes limetoa orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani namba moja ikiongozwa na Cristiano Ronaldo mshahara wake wa kila mwaka ni dola 200 milioni (Sh 518.6 bilioni) kwenye klabu ya Al Nassr, wapili akiwa mcheza gofu Jon Rahm mshahara wake ukiwa ni dola 198 milioni (513.32 bilioni.) namba tatu ikishikwa na Lionel Messi ambaye analipwa mshahara dola 65 milioni (Sh 168.8).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags