Mashatile achukizwa na walinzi wake kuwapiga raia

Mashatile achukizwa na walinzi wake kuwapiga raia

Makamu wa Rais nchini Afrika kusini, Paul Mashatile amelaani kitendo cha Maafisa wake wa ulinzi kuwashambulia Raia 2 baada ya video kuwaonesha Maafisa hao wenye silaha wakimkokota Mwanaume mmoja kutoka kwenye gari, na kisha kumkanyaga kichwani hadi kuonekana akipoteza fahamu.

Video hiyo imeibua hasira na kuangazia suala la ukatili wa Polisi dhidi ya Raia nchini humo, ambapo Mashatile ameahidi uchunguzi wa kina huku akisema anachukia matumizi yoyote ya nguvu yasiyo ya lazima dhidi ya raia wasio na silaha.

Mpaka sasa haijathibitika iwapo Makamu huyo wa Rais alikuwepo eneo la tukio wakati Walinzi wake wakitekeleza ukatili huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags