Mashabiki washambulia basi la wachezaji kwa mawe

Mashabiki washambulia basi la wachezaji kwa mawe

‘Mechi’ kati ya ‘klabu’ ya #OlympiqueMarseille dhidi ya ‘klabu’ ya #OlympiqueLyon imeghairishwa baada ya basi la Lyon kushambuliwa kwa mawe kabla ya mchezo huo na kupelekea majeraha kwa ‘Kocha’ Mkuu wa ‘timu’ ya Lyon, Fabio Grosso.

Tukio hilo lilitokea wakati ‘klabu’ hiyo ikitoka katika hoteli yao kuelekea katika uwanja wa #Velodrome kwa ajili ya pambano lao na #Marseille siku ya Jumapili nchini Ufaransa.

Inadaiwa kuwa siyo mara ya kwanza kwa matukio ya vurugu kujitokeza kabla au wakati wa ‘mechi’ za Olympique Marseille.

Mwezi uliopita polisi wa kutuliza ghasia walikumbwa na mlipuko wakati mashabiki wa ‘klabu’ ya #Marseille na ‘klabu’ ya Ajax walipopambana nje ya uwanja wa Johan Cruyff Arena kabla ya mchezo.

Mwaka jana Mashabiki wa ‘klabu’ ya #TottenhamHotspur walipata mapokezi mabaya kutoka kwa mashabiki wa Marseille kabla ya mchezo wa ‘Ligi’ ya Mabingwa Ulaya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags