Mashabiki wamtunza sidiria Burna Boy

Mashabiki wamtunza sidiria Burna Boy

Moja ya story inayotrend bado katika mitandao ya kijamii ni hii ya The African Giant Burna Boy ambaye mashabiki wa kike Jijini New York nchini Marekani walimtunza zawadi ya sidiria wakati ana-perform kwenye tamasha la 'One Night In Space' Madison Square Garden.

Mashabiki hao walifunguka na kusema kwamba wamempa Burna Boy sidiria zao baada ya kukoshwa na performance yake ambayo alikuwa akiimba live na kucheza.

Hata hivyo baadhi ya watu wengine wameoneshwa kama kukasirika na kitendo hicho cha mashabiki kwani wameeleza kuwa si lazima mashabiki hao kumtunza msanii huyo sidiria ambayo ni nguo ya ndani.

Niambie msomaji wangu kwa hapa bongo unadhani kuna msanii angekubali kuipokea sidiria kama zawadi kutoka kwa mashabiki zake za kike. Basi tuandikie maoni yako katika ukurasa wetu pale wa Instagram ambao ni @mwananchiscoop.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags