Mashabiki wamjia juu Wema Sepetu

Mashabiki wamjia juu Wema Sepetu

Baadhi ya mashabiki wa staa wa filamu nchini, Wema Sepetu wamemjia juu msanii huyo baada ya kufunguka kuwa anapendwa kupiga hasa na mpenzi wake.

Wema amepokea makombora makali kutoka kwa mashabiki wake kutokana na kauli hiyo ambayo inanekana kuwakwaza wanawake na kuchochea vipigo miongoni mwa jamii.

Kupitia katika ukurasa wake wa Instagram Wema anasema mtu kupigwa na baby wake kuna raha yake hasa pale mnapoanza kubembelezana.

"Kupigwa na baby wako kuna raha yake, haswa pale kwenye kubembelezana, ila sasa sio tupigane kama wezi kidogo tu sio mbaya halafu iwe mara moja moja sio daily, Sio lazima wote tufanane kuna wasio penda kupigwa ila as for me, kushtuashtua one time one time is very healthy jamani" amesema

Kauli hiyo ilipingwa vikali na watu huko mitandaoni na kumtaka afute kwani yeye ni kioo cha jamii hivyo hapaswi kuyasema hayo.

Hata hivyo baada ya malalamiko kuwa mengi Wema aliwajibu mashabiki zake kwa kusema “Mimi sijasema wanawake tupigwe, nimeongelea tu personally kuwa Itend to like it….but pia ukinipiga ujue unanipiga as ur lover cause the aftermath ya kubembelezana huwa ni nzuri…..

“Aaah wabongo mmezidi kunionea bwana… yaani hii kitu imekuwa turned kama ile ya mama Kanumba…. Wema asiseme kitu… kosa…!!!Asifanye kitu…kosa…!!!Ntashindwa jamnai… hata nia yangu haikuwa hiyo… nimejisemea tu kitu napenda…. Nako kosa…!!!,” alaindika.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags