Mashabiki Wamchagua Chris Brown Super Bowl 2026

Mashabiki Wamchagua Chris Brown Super Bowl 2026

Wakati mashabiki wakiendelea kumpa Kendrick Lamar maua yake kutokana na alichokifanya kwenye ‘Super bowl Half Time Show’ 2025, tayari baadhi ya mashabiki wameanza kupendekeza msanii wanayetaka akiwashe kwenye show hiyo mwaka ujao.

Kupitia Twitter ambayo sasa inajulikana kama X, mashabiki wamesisitiza Chris Brown apate nafasi ya kupafomu Super Bowl 2026 ambapo baadhi yao waliandika.

“Ninahitaji Chris Brown kutumbuiza Super Bowl Halftime Show ya 2026 ... Ni wakati." Mwingine alisema, “Jay-Z amepata kazi moja sasa. Chris Brown kwa Super Bowl 2026. Wa tatu aliongezea, "Ikiwa Chris Brown hata pafomu kwenye Super Bowl ijayo, itakuwa shida!,”

Licha ya msanii huyo kutawala chati za R&B na pop kwa takribani miongo miwili, Brown bado hajapewa nafasi ya kupafomu Super Bowl Halftime Show ambayo ni miongoni mwa heshima kubwa zinazosakwa na mastaa wengi wa muziki nchini Marekani.

Maisha ya muziki kwa Breezy yamekuwa magumu huku wengi wakiamini kuwa anakosa nafasi kubwa kama hizo kutokana na historia yake ya zamani pamoja na matukio na kesi kadhaa zilizokuwa zikimkabili.


Swali ni Je, NFL na Roc Nation ya Jay-Z itamtaja Breezy kama mtumbuizaji kwenye Half Time show ya Super Bowl 2026?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags