Watu 127 wamefariki na wengine 180 kujeruhiwa katika mkanyagano wakati wa mechi ya soka nchini Indonesia.
Inaarifiwa kuwa vurugu zilizuka kati ya mashabiki wa timu pinzani za mpira wa miguu katika uwanja wa soka wa Kanjuruhan baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Indonesia kumalizika kwa Persebaya Surabaya kuishinda Arema Malang mabao 3-2.
Mkuu wa Polisi wa Java Mashariki Nico Afinta amesema Rabsha zilijitokeza mara tu baada ya mchezo kumalizika usiku na kusababisha polisi wa kutuliza ghasia kufyatua mabomu ya machozi, jambo ambalo lilizusha hofu miongoni mwa mashabiki.
Mamia ya watu walikimbilia lango la kutokea katika juhudi za kukwepa mabomu hayo, wengine walikosa hewa katika vurugu hizo na wengine kukanyagwa, huku Watu 34 wakifariki papohapo.
Wengine zaidi ya 300 walikimbizwa katika hospitali za karibu kutibu majeraha lakini wengi walikufa njiani na wakati wa matibabu, idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka, kwani takribani Watu 180 wako katika hali mahututi.
Leave a Reply