Mashabaiki wamshitaki Madonna

Mashabaiki wamshitaki Madonna

Msanii wa Pop kutoka Marekani, Madonna amefunguliwa mashitaka na mashabiki wake kutoka #NewYork baada ya kuchelewa kupanda jukwaani katika tamasha lililofanyika Disemba mwaka 2023.

Mashabiki hao waliotambulika kwa majina Michael Fellows na Jonathan Hadden walifungua kesi ya madai ya mazoea mabaya na udanganyifu katika Mahakama ya #Brooklyn wakieleza kuwa ‘tiketi’ za tamasha hilo ziliandikwa muda wa kupanda ‘stejini’ wa Madonna ni saa 2:30 usiku lakini alipanda saa 4:30 usiku.

Kufuatiwa na shauri lililopelekwa Mahakamani limeeleza kuwa Mashabiki hao wamedai kuwa walikumbana na changamoto kutokana na tamasha hilo kuchelewa kuisha zikiwemo kuchelewa kazini siku inayofuata na kupata gharama kubwa za usafiri wa umma baada ya tamasha hilo kuisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags