Imetimia Miaka 2 Tangu Costa Titch Afariki

Imetimia Miaka 2 Tangu Costa Titch Afariki

Imetimia miaka miwili tangu mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Costa Titch afariki dunia ambaye alifariki baada ya kuanguka jukwaani wakati alipokuwa akitumbuiza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram umeendelea kumkumbuka msanii huyo kwa kushare baadhi ya kazi zake mbalimbali ambapo katika siku hii wakichapisha ujumbe wa kumtakia aendelee kupumzike kwa Amani.

“Leo inatimiza miaka miwili tangu Costa alituacha, lakini hakuna siku inayopita bila kuhisi uwepo wake. Shauku yake, na upendo alioutoa kwa dunia bado vinaishi kupitia muziki wake na harakati aliyojenga.

Kwa kila mtu anayeendelea kusherehekea maisha yake na urithi wake asante. Upendo na msaada wenu vinamaanisha kila kitu kwetu. Tuendelee kuuhifadhi jina lake,” imeandika taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram

Costa Titch alijipatia umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake za Amapiano na hip hop, zikiwemoNkalakatha, Big Flexa, Activate, Superstar, Shetani.

Msanii huyo alizaliwa September 10, 1995 alifariki dunia 2023, akiwa na umri wa miaka 28 wakati alipokuwa akitumbuiza katika jukwaa la Puppy Park kwenye tamasha la ‘Utra Music’ mjini Nelspruit, Afrika Kusini.

Utakumbuka mwezi Mei mwaka jana familia iliweka wazi sababu ya kifo cha msanii huyo ambapo kulingana na majibu ya uchunguzi kutoka kwa mtaalamu wa magonjwa maalumu ya (Human tissue) Costa alipata mgandamizo mkubwa katika moyo wake.

Mtaalamu huyo amefafanua hali hiyo ambayo haikujulikana ilianza lini kwa Costa ambayo ilisababishwa na msongo wa mawazo, uchovu wa muda mrefu na kupelekea mapigo ya moyo kwenda kwa kasi isivyo kawaida na kupelekea kifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags