Masele: Mlevi akilewa anakosa balance ya nyuma

Masele: Mlevi akilewa anakosa balance ya nyuma

Mchekeshaji Chrispin Masele maarufu ‘Masele Chapombe’ amefunguka kuhusu yeye kuhusishwa kutumia vilevi kutokana na kuyumba pale anapoigiza ambapo amesema anaweza akanywa akijisikia.

Masele ambaye alifanya mahojiano maalumu na Mwananchi Scoop amesema “Mimi siyo mlevi lakini ni binadamu naweza nikanywa nikijisikia sipo sana kwenye ulevi lakini napenda kukaa na watu wanaokunywa pombe kwa sababu maneno mengi yapo baa, watu wananiita baa wananinunulia, ili nisiwaangushe nawadanganya natumia dawa.

Amesema mwaka huu kuna mtu alimualika kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto wake ili akachekeshe lakini wale watu walidhani ni mlevi wakanunua kreti tatu za bia ambapo alibidi adanganye anatumia dawa.

“Mimi nimeingia kwa undani kujua pombe ni nini kabla ya kuigiza ulevi nilifanya ‘research’ kujua pombe ni nini nikapata mtaalamu mmoja akanielekeza akaniambia unapokunywa bia ‘alcohol’ yake inazunguka kwenda nyuma yaani mlevi yeyote wa bia huwa anakosa ‘balance’ ya nyuma, waangalie wengi wanadondoka kwa kukaa,”alisema.

“Mlevi wa pombe kali ‘alcohol’ inazunguka kwenda mbele hana ‘balance’ ya mbele, ndiyo maana wengi wana makovu usoni lakini mtu anayechanganya anakosa ‘balance’ zote ndiyo unakuta kashikiliwa au anabebwa kwa hiyo na mimi nikajua jinsi ya kuyumba kutokana na chupa ya pombe niliyoshika,” amesema.

Aidha mchekeshaji huyo ambaye kwa saa amerudi kwenye gemu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu amesema familia na uuzwaji wa kazi zao kiholela ulifanya atulie kufanya kazi ya sanaa.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post