Marumo wagoma kufanya mazoezi

Marumo wagoma kufanya mazoezi

Ikiwa ni siku moja tuu imebaki ili timu hiyo iweze kuingia ndimbani kwa ajili ya mchezo wao na mabingwa mara 29 yanga Afrika, wachezaji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini wamegoma kufanya mazoezi mchana huu kwa sababu hawajapata bonasi waliyoahidiwa.

Timu hiyo kesho itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng saa 12 jioni kwa muda wa Afrika Kusini sawa na saa 1 usiku Tanzania.

Chanzo cha wachezaji hao kugoma na kukaa hotelini walipoweka kambi ni kutopata bonasi ya Sh1 bilioni ambayo waliahidiwa na uongozi wakivuka nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa jarida la FARPost wachezaji hao si mara ya kwanza kufanya hivyo kwani mechi ya robo fainali dhidi ya Pyramids FC walitishia kugoma ila baada ya mazungumzo walikubali kuingia uwanjani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags