Marufuku wenza wenye watoto kuachana

Marufuku wenza wenye watoto kuachana

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga katika uzinduzi wa zahanati katika kijiji cha Mpona mkoani humo amesema kuwa wenza (wapenzi) wote wenye watoto hawatakiwi kuachana  badala yake wanatakiwa kuwa pamoja kulea watoto.

“Haiwezekani umzalishe binti halafu umuache kwa kuwa amefubaa au amebadilika kwani ulivyo taka kumzalisha ulifikiria kuhusu mabadiliko” alisema Queen

Aidha amewaagiza viongozi wa serikali za vijiji na kata mkoani hapo kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola vijana wote watakaobainika kushindwa kulea watoto na kuzitelekeza familia zao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags