Marufuku watoto kucheza ‘show’ kwenye masherehe

Marufuku watoto kucheza ‘show’ kwenye masherehe

Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa onyo  watoto kutoruhusiwi kucheza ‘show’ kwenye masherehe hasa nyakati za usiku, ni kufuatia kusambaa kwa video mbalimbali kwenye mitandaoni ya kijamii, zikionesha watoto wakitoa burudani kwenye Sherehe wakati wa usiku na katika miondoko isiyofaa kwa umri wao.

Waziri huyo ameeleza kuwa watakaa kikao na chama cha washereheshaji nchini na wadau wote ambao kupitia shughuli zao wanaweza kusababisha kuvunjwa kwa sheria hiyo ili kuzungumzia mchango wao kwenye kulinda maadili ya watoto katika kazi zao kwa mujibu wa sharia.

Aidha sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 iliyorekebishwa mwaka 2019, inazuia kumtumia mtoto kwenye maonesho ya harusi, maonesho ya mitindo ya nguo au maonesho mengine kama hayo wakati wa usiku. Adhabu yake ni faini ya tsh laki tano au kifungo cha miezi 6 jela au vyote kwa pamoja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags