Baraza la Madiwani Jijini Mbeya limesitisha usajili mpya wa Usafiri wa Bajaji kutokana na kuwa nyingi jijini humo kuliko Mahitaji pamoja na kusababisha Ajali mara kwa mara.
Mfumo wa Usajili umefungwa hadi wakati ambapo Miundombinu itakapokuwa rafiki kwa matumizi. Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Triphonia Kisiga amesema Bajaji zilizosajiliwa Mkoani hapo ni 3000
Naye, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mohamed Issa amesema “Mbeya imekuwa kama dampo la Bajaj, imefika hatua tunasema Hapana.”
Leave a Reply