Marufuku kuwalaza watoto chumba kimoja na wageni

Marufuku kuwalaza watoto chumba kimoja na wageni

Taarifa kutoka mkoani Tanga ambapo Wazazi na walezi Mkoani humo   wametakiwa kuacha tabia ya kuwalaza watoto wao na wageni mbalimbali majumbani ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Magaoni Jijini Tanga Mohamed Rajab wakati wa Bonanza la tulivu magaoni lililofanyika kwa lengo la kuzuia vitendo vya uhalifu na mambo maovu katika kata hiyo.

Vitendo hivyo  ambavyo wamekuwa wakifanyiwa watoto wengine ikiwemo ulawiti ambapo wmeaswa kujenga utaratibu wa kuwakagua watoto wao hali zao za kimwili pindi wanaporejea kutoka mashuleni ili kuwalinda na vitendo hivyo.

"Hata Mgeni akija, Sio rahisi mjomba akalale na mtoto wako huko ndani. Atalala na mtoto wako atafanya uharibifu halafu asubuhi anaondoka huku mtoto amemwamwachia uharibifu" Amesema Diwani Rajabu.

Diwani Rajab amesema wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwaamini wageni wanaokwenda kuwatembelea majumbani na hatimaye kuwaacha wanalala na watoto wao huku wakisahau jukumu la ulinzi wa mtoto ni la Mzazi pekee.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags