Marufuku kutumia TikTok

Marufuku kutumia TikTok

Serikali ya Nepal imepiga marufuku matumizi ya mtandao wa kijamii wa TikTok kutokana na tuhuma za kuwa inavuruga maelewano ya kijamii huku zaidi ya kesi 1,600 za uhalifu wa mitandao zimewasajiliwa ndani ya miaka minne iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal Narayan Prakash Saud amesema uamuzi wa kuupiga marufuku mtandao huo unaanza mara moja baada ya mkutano wa Bunge uliofanyika Jumatatu.

Aidha Waziri huyo aliongeza kuwa ili mitandao ya kijamii iweze kuwajibika serikali inataka makampuni kujisajili nchini humo, kulipa kodi na kufuata sheria na kanuni za nchi hiyo.

Mtandao wa TikTok unaomilikiwa na kampuni ya ByteDance ya China umekuwa ukikabiliwa na migogoro katika nchi mbalimbali kutokana na wasiwasi kuwa Beijing inaweza kuwa inautumia mtandao huo kukusanya taarifa binafsi za watumiaji kwa maslahi yao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post