Marufuku kuingia bungeni na kaunda suti

Marufuku kuingia bungeni na kaunda suti

Bunge nchini Kenya limepiga marufuku uvaaji wa suti iliyopewa jina la aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Kenneth Kaunda ndani ya jengo hilo.

Spika wa Bunge, Moses Wetangula amesema suti za Kaunda, pamoja na nguo za asili za Kiafrika, hazitakiwi kuvaliwa bungeni. Huku akiitaja marufuku hiyo kuwa ni matokeo ya mitindo mipya ya mavazi ambayo ilikuwa changamoto kwa kanuni iliyowekwa ya mavazi bungeni.

Hata hivyo Rais wa nchi hiyo William Ruto mara kwa mara huvaa Kaunda suti wakati wa hafla rasmi, na hivyo kuchangia umaarufu wake kwa wasomi wa kisiasa siyo tu nchini Kenya lakini pia katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags