Martin Kadinda:  Mwanamitindo Mwenye Kipaji cha pekee

Martin Kadinda: Mwanamitindo Mwenye Kipaji Cha Pekee

Na Jacqueline Mandia

 Martin Kadinda ni Mwanamitndo maarufu sana katika tasnia nzima ya mitindo nchini Tanzania, Kijana huyu aliianza safari yake katika ulimwengu wa mitindo mnamo mwaka 2007hadi 2010 na hapa alikuwa mwanamitindo wa jukwaani na si mbunifu na katika safari yake hiyo alifanikiwa kushinda tuzo kama mwanamtindo mwenye kipaji Zaidi (2008) wakati (2010) alishinda tuzo ya mwanamitindo bora wa kiume.

 Kuvutiwa kwa Martin katika mitindo kulianzia kuonekana kutokana na kuwa na jicho la kupangilia mavazi akiwa na umri mdogo sana na ikaongezeka hadi kufikia kuwa ambaye sasa ni mbunifu wa kimataifa wa mitindo, kocha, jaji, mshauri, na mtu anayechangia katika miradi ya ushawishi katika miradi ya ushawishi katika jamii.

 Safari  yake ilianza mara baada ya kujiunga na tasnia ya uanamitindo Tanzania kati ya 2007 na 2010 akionyesha mafanikio ya haraka kutokana na kushinda taji la ODEL mwenye vipaji Zaidi mwaka 2008 na Model mwenye  vipaji bora mwaka 2010 na kuibua njia mpya iliyoletea mafanikio katika taaluma yake.

Akiwa na miaka  22 Martin Kadinda aliamua kubadili muelekeo wake kutoka kuwa mwanamitindo maarufu jukwaani na kuweza kuwavalisha wanamitindo mbalimbali, na aliweza kupata bahati ya kumvalisha mwanamitindo maarufu kabisa kwa jina la NAOMI CAMPBEL, na mpaka sasa anawavalisha watu maarufu nchini.

 Kutokana na maamuzi ya kuanza kuwavalisha watu maarufu Martin Kadinda aliweza kutoa collection yake iitwayo Blazer Single Button amayo ilimpa sna jina kwasababu hakuna mtu maarufu ambaye hakuivaa na  hii ilimpa tuzo ya best Menswear Designer of the year.

Hata hivyo Mwanamitindo huyu hakuishia hapo bali aliweza kuleta tena collection nyingine iliyoitwa kwachu kwachu.

 Mwanamitindo wa Tanzania Martin Kadinda alizidi kupata umaarufu papo hapo mara baada ya kumvisha mwanamuziki anayefanya vizuri Zaidi Afrika Mashariki Diamond Platnumz kutokana na video yake ya Muziki (mawazo) . Fursa hiyo ilisababisha kutambuliwa kwa kazi yake kwa kiasi kikubwa na hivyo kufungua didrisha kwa wateja ndani yaTasnia ya burudani ndani nan je ya nchi. 

Habari zilienea haraka sanaa kwa kazi  yake kupitia miundo ya kipekee na hivyo kupanua wigo wa wateja wake mbali na viongozi mashuhuri wa serikali kama Mhe.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, International super Millen Magese, Big Brother Africa akiwadhihirisha Washindi Uti Nwachkwu, Idris Sultan, Mwanasaksafoni wa UNIMAGIBALE wa Uganda Brian Mugenyi na mbunifu wa vito wa Nigeria Monalisa kwa kutaja machache.

 Kufanya kazi na watu wengi kumempa Martin Kadinda fursa ya kujitambulisha moja moja na kujihusisha na jamii kwa ujumla. ni kwa njia hii kwamba anaendelea kushughulikia mahitaji ya kijamii na athari endelevu,Kazi za Martin zinzaonekana katika miradi kadhaa ya kubadilisha maisha kama jaji, kocha na mshauri.

Martin ni balozi mwema wa FASDO Tanzania, shirika linaloibua vipaji vya vijana kupitia Sanaa na bandari  hadi sasa.

Mbali na hapo Martin Kadinda ameweza kufanya kazi na wanamitindo  wa kitanzania kwa kutumia vitambaa dizaini ya khanga ambavyo vina ujumbe wa kuhamasisha afya ya uzazi na usawa wa kijinsia kilichopo chini ya Tanzania Bora Initiative na pia bingwa wa onyesho la mitindo la Beyond Fashion  ili afyaya mama na motto kufikia jumla ya watu 4,000 katika mikoa mine ya watanzania yenye huduma ya uchunguzi chini ya TAHMEF.

 Vilevile chapa ya “Just MK” mavazi imeweza kuzindua kampeni nyingine nyingi zenye athari za kijamii zikiwemo Tamasha la Giving is Fun ambalo lilisaidia kuwafikia wanafinzi 1,000 wilayaani kibondo wakiwa na vifaa muhimu vya shule na pia RedRibbon kuchangia fedha za kuboresha ustawi wa watoto wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI kuoitia elimu, afya na malazi.

 Mwanamitindo Martin Kadinda anautofauti mkubwa na wanamitindo wengine kwani karibia kila mwaka huweza kuja na wazo ambalo litafurahisha watu na kuwafanya wapendeze, hata hivyo muongozo uliopo katika chapa ya “Just MK” unapanga kuanzisha na kuboresha mitindo yake na pia inaonekana kufungua mipaka mipya kupitia maonyesho  kwenye hatua kubwa Zaidi, kupokea tuzo nyingi Zaidi na kuweza kutambuliwa ulimwenguni kote.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.


Latest Post