Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Marioo amemtambulisha Stans Ooh kama msanii wa kwanza kwenye lebo yake ya 'Bad Nation'.
Msanii huyo ametambulishwa mapema leo Agusti 29, ikiwa ni baada ya Marioo kuchapisha tangazo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimkaribisha msanii huyo mpya 'Bad Nation'
Marioo anaenda kuongezeka katika orodha ya wasanii wenye lebo nchini ambapo kati ya zilizotangulia ni Wasafi Classic Baby (WCB) ya Diamond Platnumz, Konde Gang ya Harmonize, King Music Alikiba, African Princess ya Nandy, Next Level ya Rayvanny na nyinginezo.
Uongezekaji wa lebo hizo unaonesha ukuaji wa wasanii husika wanaomiliki lakini. Si hiyo tu lakini pia lebo zimekuwa zikisaidia wasanii katika kusimamia kazi zao upande wa matangazo na kufanya ziwafikie zaidi wapenzi wa muziki duniani kote.
Hata hivyo kwenye upande wa shoo za wasanii lebo zinaweza kusaidia katika kupanga na kuratibu matukio kama vile shoo za moja kwa moja, tamasha, na ziara za muziki. Hii inasaidia wasanii kufikia mashabiki wao moja kwa moja na kuongeza umaarufu wao.
Kwa hiyo, lebo za muziki zinamchango mkubwa katika maendeleo ya kazi za msanii, lakini pia ni muhimu kwa wasanii kufahamu masharti ya mkataba yao na kuhakikisha kwamba wanapata sehemu ya haki katika faida zinazopatikana.
Leave a Reply