Marekani kuleta intarnet kwa gharama nafuu nchini

Marekani kuleta intarnet kwa gharama nafuu nchini

Weeeeeh! Vip hii imeshakufikia au bado, kama nawaona wenzangu na mie wapenda kuweka status nyingi huu ni muda wetu sasa basi bwana unaambiwa…

Serikali kutoka nchini Marekani kupitia idara ya biashara na maendeleo imesema itasaidia kupanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya intaneti kwa gharama nafuu kwa maelfu ya watu katika nchi za Afrika Mashariki na Kati ambazo ni Tanzania, Kenya, Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo na Uganda.

Ikumbukwe tu wakati wa mkutano wa Aprili 2022, Rais Samia na Makamu wa Rais Harris waliahidi kujielekeza katika kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania katika maeneo ya usalama wa mtandao na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

Akiongea Ikulu jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema

“Toka wakati huo Marekani imefanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania kuendesha warsha ya kikanda kuhusu TEHAMA, imetoa msaada wa kitaalamu kuhusu teknolojia ya 5G, usalama wa mtandao, na kupambana na uhalifu mtandaoni, pamoja na kuwezesha uwekezaji mkubwa zaidi wa wawekezaji wa Kimarekani katika sekta ya TEHAMA nchini Tanzania” amesema Kamala







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags