Mapya yaibuka aliejifungua mtoto na kugeuka kuwa jiwe

Mapya yaibuka aliejifungua mtoto na kugeuka kuwa jiwe

Amina Rashidi mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa Kijiji cha Mwabuki wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, amabe amedai kuwa mtoto wake mchanga amefariki dunia na kugeuka kuwa jiwe.

Amina alifikia uamuzi huo baada ya mwanaume aliyempa ujauzito kutaka amzalie mtoto wa kiume, la sivyo asingeweza kumtunza kwani hitaji lake lilikuwa ni mtoto wa kiume na sio wa kike.

Kutokana na hitaji hilo la mwanaume huyo, aliejulikana kwa jina la Hamisi, mzaliwa wa Mkoa wa Mara na mkazi wa jijini Dar es Salaam, Amina aliendelea kumhakikishia mwanaume huyo kuwa lazima angemzalia mtoto wa kiume.

Machi 17, katika Zahanati ya Kijiji cha Mwabuki, mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike hivyo kufifisha ndoto zake za kupata huduma kutoka kwa mzazi mwenzie kama alivyoahidiwa.

Baada ya kujifungua mtoto huyo wa kike, mama huyo alitoa taarifa kwa mzazi mwenzie kuwa amejifungua mapacha mmoja wa kike na mwingine wa kiume ambaye alifariki dunia na kugeuka jiwe, hali iliyosababisha taharuki kubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags