Mandonga mtu kazi amjibu Shabani Kaoneka

Mandonga mtu kazi amjibu Shabani Kaoneka

Alooooooooh! Wasawahili wanasema vita ni vita hahahaha! Make hapa  kwanza ncheke basi bwana ukiachana na swala la simba kuna hili balaa jingine huko mjini Instagram watu sasahivi wanapigana kwa maneno kwanza ngumi wamezipumzisa kidogo.

Karim Mandonga aamjibu bondia mwenzake aliempiga raund ya nne tu Shabani Kaoneka baada ya jana kulalamika kuwa yeye alieshinda anakuwa maskini na Mandonga aliepigwa anakuwa tajiri, mtu kazi aliamua kufunguka na kuandika kuwa

“Dah shabani ndugu yangu me naamini kabisa ridhiki inatoka kwa mafungu na kwa muda maalumu alieupanga mungu suala la nani afanikiwe nani aishie njiani ni majukumu ya Allah mimi na wewe hatupaswi kumlaumu mtu yoyote yule” aliendelea kwa kusema

“katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi na watu wa media kiujumla hata mimi sijawah kuwaza kwamba ipo siku nitasimama kama superstar mkubwa but all in all tujfunze kumshukuru mungu kwa kila jambo. Kama ipo ipo tu” ameandika Karim Mandonga






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags