Manara: Sitaki tena mpira

Manara: Sitaki tena mpira

Aliye kuwa msemaji  wa ‘klabu’ ya #Yanga Haji Sunday Manara amefunguka kuachana na masuala ya mpira na kutouzungumzia kabisa, akidai mpira umejaa uadui.

Akizungumza na waandishi wa habari , Manara amesema hivi karibuni ataitisha mkutano na waandishi ili kutangaza kuachana na mpira, akidai kuwa mpira umejaa uadui mkubwa na ukubwa wa jina lake unasababisha watu wengi watengeneze uadui naye. Lakini  pia hakuacha kuitaja sababu ya mambo ya usimba na uyanga.

Alienda mbali zaidi kwa kusema akiachana na masuala ya mpira na ushabiki kutaepusha familia yake na vifo visivyotarajiwa na kama akiendelea kubaki kwenye mpira ipo siku watu watashuhudia wakimzika bila sababu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags