Manara: Nimemkumbuka Ex wangu muungwana

Manara: Nimemkumbuka Ex wangu muungwana

Kama inavyo fahamika  kila ifikapo siku ya Alhamis baadhi ya watu hu-post picha zao za zamani kwa ajili ya kukumbuka siku hizo, kwa aliyekuwa msemaji wa ‘klabu’ ya Yanga Haji Manara amem-post aliyekuwa mke wake na kuandika kuwa ndiyo TBT yake ya leo.

Kwenye picha hiyo Manara ameandika,

“Tbt, hata kama tumeachana bado anabakia mtu muhimu ninayemkumbuka mara kwa mara kwa ucheshi wake na kujali kwake. Ni yeye baada ya kuachana naye akanivuruga nikawa naoa kama kuku, nathubutu kusema binti huyu aliniingia mno moyoni.

Uzuri wake hatukuachana vibaya ni sababu za kijingajinga, mimi hadi leo sikumbuki nini kilitokea. Mtu mzuri na anakufanya uwe busy na mahusiano, active mno nyumbani, mcheshi kwa wageni na hana mbwembwe, kisha yupo kando na mitandao kabisa, kwake anaitumia kibiashara tu.

Kiufupi atakayemuoa huyu kalamba turufu. Ahhh nimemkumbuka tu X wangu huyu m uungwana.Kila la kheri mtu aliyenipa jina la Bugati ukasema wewe ni Bugati,ukanipenda mimi mwenyeww siyo umaarufu wangu wala nilichonacho, najua yashamwagika ila wallah naku-miss".
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags