Manara awajia juu TFF baada ya kumpiga stop Kisinda

Manara awajia juu TFF baada ya kumpiga stop Kisinda

Hellow! It another Monday mtu wangu wa nguvu, I hope mko good kabisa, leo katika michezo bwana yule msemaji aliefungiwa miaka 2 na faini Haji Manara, ametoa povu baada ya Tff kumpiga stop winga wao waliomtambulisha hivi karibuni.

Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Kumzuia Tuisila kisinda kucheza Yanga Kwa sababu zisizokidhi masharti ya kanuni ni mwendelezo wa uonevu dhidi yetu, Kosa lipo wapi wakati usajili wake umewahi kabla dirisha halijafungwa? Mwisho lini Club kupangiwa muda wa kuwasilisha majina ya usajili? Iwe Kwa Wachezaji local au foreigners?” Haji aliendelea kwa kufunguka kwa kuandika

“Kamati inayohusika na Hadhi za Wachezaji imekaa lini hadi Katibu utoe hukumu?Tunafanya hv vtu kumfurahisha nani?, Kwa Interest ya kina nani? Taarifa:Wananchi, Tff bila sababu zenye mashiko,imezuia usajili wa Winga wetu Tuisila Kisinda kusajiliwa Yanga ,ilhali tumewahi deadline ya mwisho ya kabla dirisha la usajili kufungwa” ameandika Manara

Sio hayo tuu msemaji huyu akiamua kuongea huwa anaongea kweli kweli aliendelea kwa kutoa maelezo kuhusiana na timu yao kuwasilisha majina mapema kabla ya usajili kufungwa na kusema kuwa “Club imewasilisha Majina ya Wachezaji kumi na mbili wa kigeni watakaocheza msimu ujao,jina la Tuisila likiwemo kabla dirisha halijafungwa,,Why Katibu ujipe jukumu la kamati ya hadhi za Wachezaji na kuandika Barua ya maamuzi? Kwa nn usisubiri maamuzi ya Kamati? Uharaka wa nn?” ameandika Manara

Aidha alihitimisha kwa kuandika kuwa “Hiki kiburi kimetokea wapi? Mnajisikiaje Kila siku kuifanyia hv Yanga?, ITC anayo,kawahi deadline,Why mnatutendea hivi, Yanga imekuwa mnyonge nchi hii?, No No No No ,,imezidi sasa, Kwa ilivyo ,,ndio Tuisila hachezi hvyo na hatuna la kufanya Mamlaka ishaamu” ameandika Haji Manara


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post