Man United yaisaka saini ya beki wa Bayern

Man United yaisaka saini ya beki wa Bayern

Tetesi zinadai kuwa klabu ya Manchester United wako mbioni kuisaka saini ya beki wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Uholanzi, Matthijs De Ligt.

Inaelezwa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka miaka 24 tayari yupo katika hatua ya awali kufanya makubaliano na Manchester United. Huku ikidaiwa kuwa Man U wako tayari kumpa De Ligt, mkataba wa miaka mitano ikiwa mambo yataenda kama inavyotarajiwa.

Matthijs De Ligt ambaye kwa sasa yupo katika timu yake ya taifa ya Uholanzi kwenye fainali za Euro 2024 aliingia Bayern Munich mwaka 2022 kwa mkataba wa miaka 6.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post