Mambo yanayozuia mafanikio katika biashara yako

Mambo yanayozuia mafanikio katika biashara yako

Mambo vipi watu wangu wa nguvu? Kama kawaida yetu katika segment ya biashara hatujawahi kuwa na mba mba mba so leo nitaongea kwa ufupi sana ili kila mtu apate kuelewa.

 

Katika biashara yako bwana kuna vitu ambavyo kwa upande wako wewe unaweza kuvidharau lakini ndivyo hivyo vitakavyo haribu biashara yako isiweze kufanikiwa.

 

Mafanikio/kufanikiwa katika biashara yako kwanza kabisa kunaendana na wewe tabia ulizonazo, na hizi ni baadhi tu ya sababu za kutofanikiwa katika biashara yako…

 

  • Kukosa maarifa ya kutosha ya fedha

Siku zote fedha inahitaji maarifa fulani kwenye namna ya kuingiza, kuwekeza pamoja na kusimamia fedha. Sasa watu wengi hawana hii financial literacy au financial knowledge.

Katika biashara yako unahitaji sana maarifa katika utumiaji wa pesa yako sio unatumia tu, ndo maana katika biashara inabidi uwe na daftari ambalo utaandika kila kitu kinachotoka na kuingia ili biashara yako isiweze kuyumba.

  • Aina ya marafiki

Kuna aina ya marafiki kama ukiwa nao wanaweza wakapelekea kujikuta nawe ukipoteza hela zako. Haswa wale wasio na nidhamu ya fedha ambao ni wapenda kufanya anasa na matumizi yasiyo na mpangilio.

Sio kila rafiki kwako basi ana nia nzuri na wewe au anakutakia mema. Kuna baadhi ya marafiki hata hicho kidogo unachokifanya kwa ajili ya kukunufahisha hawapendi, basi watatumia muda huo kukufanya uwe mchafuzi wa fedha zaidi ili ufilisike, so ukiwa mfanyabiashara kuwa makini na marafiki ulionao. Wengine watapendezwa na unachokifanya .

  • Kutokuwa na bajeti

Bajeti ni kama vile ramani kwa mtu ambayo humuongoza kuhusu kufanya matumizi yake. Tabia ya kuwa na bajeti ndiyo inamsaidia mtu kufanya matumizi yake kwa kimahesabu na kuepuka matumizi mabovu ya pesa.

Ukichagua kuwa mfanyabiashara basi cha kwanza ni kuwa na nidhamu ya pesa na pili kuweka bajeti so ukitaka biashara yako isitetereke basi jifunze kuwa mtu mwenye bajeti sana.

  • Kuendekeza tamaa

Pesa haiongozwi kwa matamanio (tamaa) la sivyo itaishia kuteketea na kupotea kwa upesi sana. Pesa inabidi iongozwe kwa fikra, yaani iwe inatumiwa kwa mipango na kufikiria kwa umakini sana ili kuepuka matumizi ya tamaa.

Kwenye biashara bwana hakutaki tamaa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wanakuwa na tamaa zisizofaa, embu tulia na biashara yako hiyo moja sio leo unataka kuuza hichi kesho hichi, ukiona rafiki yako kafungua hichi na wewe unataka, embu punguza tamaa ili upate mafanikio upesi kwa hicho unachokifanya na kukiamini.

Cha kuzingatia katika biashara acha kuendekeza tamaa na kufuata mikumbo itakufanya uchelewe kufanikiwa na sio kwenye biashara tu, hata kwenye maisha yako ya kawaida.

  • Kupenda starehe

Siku zote waswahili wanasema starehe ni gharama. Kama ukiwa ni mtu wa kuendekeza starehe basi fedha zako zipo hatarini sana kupotea kwenye matumizi ya gharama za kumudu starehe hizo.

Kuna baadhi ya starehe sio za lazima sana ambapo kama mtu usipojizoesha sana kupenda starehe unaweza kujikuta ukiokoa pesa zako nyingi sana kutopotea.

Na hii nimezungumza kwasababu kama wewe ni mfanyabiashara unategemea pesa za matumizi kutoka kwenye biashara so ukisema hizo pesa unazozipata utumie kwenye starehe basi hautaambulia kitu chochote katika mzunguko wako wa pesa.

  • Kutokuweka kuweka akiba na uoga wa kupata hasara

 

Akiba ni muhimu sana katika kuokoa pesa zako, hivyo kama haufanyi savings kuna uwezekano mkubwa wa kuishia kupoteza hela zako za ziada.

Tabia ya kuwa na uoga inaweza kumpelekea mtu kutofanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya pesa zake sababu ya uoga wa kufilisika, mtu anaacha kuwekeza pesa yake na kuishia kuifanyia matumizi ya starehe nyingine.

Usiogope kupata hasara kwenye biashara, jambo la kwanza unatakiwa kufikiria ni hasara na sio faida

I hope tumeelewana wafuatiliaji wa @Mwananchiscoop, endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii na magazine zetu kwa ajili ya kujifunza zaidi na zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags