Mambo yanayoweza kukuvunjia heshima kazini

Mambo yanayoweza kukuvunjia heshima kazini

Mambo vipi!!!wanetu sana  najua mko swalama kabisa kama kawaida yetu sisi lengo letu mahususi kabisa ni kukuhabarisha yale usio yajua na unayo yasikia mwananchi scoop inakujuza zaidi au vipi mwanetu.

Leo katika kipengele cha kazi weekend hii tutazungumzia mambo ambayo yanaweza kumfanya mtu akapoteza heshima kazini.

Kitu cha kwanza ambacho mtu unatakiwa kuwa nacho katika kufanyaji kazi ni nidhamu nzuri na kuwa ubora kazini hii humuongezea mtu credit na kuaminika katika ufanyaji kazi kuanzia bosi hadi wafanyakazi wakikuona lazima watakupa heshima yako kwa namna ya kipekee sana kutokana na nidhamu ulio itengeneza hapo awali.

Sasa Mwananchi Scoop tutakufafanulia zaidi yawezekana kuna jambo unaendelea kulifanya ofisini mpaka sasa hivi kumbe lina kushushia heshima na haujui mwanetu.

  • KUTUMIA LUGHA ZISIZO RASMI OFISINI

Hapa ndio kuna umuhimu sikuzote sehemu za kazi unatakiwa uchunge mdomo wako na maneno machafu katika kila kitu kumbuka kuishi kwa tahadhari hata katika kuongea na wafanya kazi wezako.

Hata kama kuwe kuna jambo limekukwaza usitumie lugha chafu kama kutukana, kukashifu mtu, lugha za kejeli au kutumia lugha za mtaani yaani kama muhuni Fulani wakati upo sehemu ambayo ahusiani na vitu unavyo visema.

  • KUVAA MAVAZI YA SIO FAA KAZINI

Hili suala limebezi sana kwa wanawake wamekua wakiukaji wa mavazi kazi kisa kuendana na utandawazi lakini kazi stara ya mavazi ina muheshimisha mtu nakuonekana smart na mtu mwenye akilib pengine ukawa mfano wa kuigwa unaweza kuta ofisini binti amevaa nguo za. kubana au sketi fupi ni rahisi kujishua heshima kuonekana muhuni so kwa hivyo huwezi kuwekwa kipaumbele kazini .

  • KUWA MKOROFI KAZINI

Ukorofi imekuwa kitu cha kawaida hasa kwa mabosi ukiuliza kikundi cha wafanyakazi, ‘unaridhika na bosi wako? , litakuwa si jambo la kushangaza wengi wao watakapo kujibu, ‘hapana’. Ingawa unaweza kufikiri kuwa wafanyakazi wengi hawapendi mabosi wao kwa sababu tu wanawapa kazi nyingi za kufanya.

Na pale wanapokosea wanakemewa, lakini ukweli ni kwamba, wengi hawaridhishwi na mabosi si kwa sababu ya kazi wanazotupa, bali sababu ya tabia zao na hupelekea kuwashushia heshima katika kazi.

Kwa upande mwengine unakuta mfanya kazi anakuwa kero kwa mfanya kazi mwenzake ili mradi tu amtoe kwenye mood ya kazi hapo wezi kupata heshima au kuwa natabia ya kuwatongoza wafanya kazi wenzio muda wakazi, kupiga umbea na kumsumbua mfanya kazi mwenzio wakati anapo fanya majukumu yake.

  • KUWA NA SIFA ZISIZO NA MAANA KAZINI

Kuna msemo ambao unasema kwamba, ukitafuta heshima kwa gharama ya juu basi utapata dharau kwa bei nafuu msemo huu unamaanisha siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwaajili ya kusifiwa au mazungumza ya kujivunia.

Lazima utadharaulika kwa sababu utafanya mambo kupitiliza tena mengine ya sio faa kwa kutaka sifa hapo hadhi yako lazima ishuke tena watakutunga jina mzee wa misifa huyo ana kuja.

  • KUTOTIMIZA AHADI

Ukiwa mtu wakuahidi mambo halafu utimizi hii ina kupelekea kuwa muongo muongo na moja ya kuheshimiwa ni kusikilizwa na kuaminiwa juu ya jambo unalo lizungumza kwa wakati huo mfano wafanya kazi. .wenzio wakasema ‘achana nae huyo hana la kusema mzugaji tu’hapo mwamba ukiona hivyo huna respect utakayo pata.

Ila tu nikwambie kitu mwanangu sana kama una moja ya mambo hayo kazini na unataka uheshimiwe unao muda wa kujisahihisha chukua hatua badilika kwasababu kupewa jina la mzee wa busara sehemu za kazi ujue kunaheshima aliitengeneza huyo mtu na kupachikwa jina hilo.

Watu kutamani kumsiliza na kumshirikisha kwenye mambo mbali mbali ya ofisini na hata ya kibinasfi kwasababu mtu anajua akimshirikisha Fulani jambo lake atamshauri vizuri kwa kuwa ana hekima na busara amabayo ilitokana na kujiheshimu, akili mtu wangu.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post