Mambo yanayosababisha mwanaume kuwa mdhaifu kitandani

Mambo yanayosababisha mwanaume kuwa mdhaifu kitandani

Uwiiiiiiiiih! Inabidi mzoee tuu mana sasahivi tumekuja kivingine katika mahusiano yani Atari na nusu mada zetu ni konki na zitakufunza mambo ambayo ulikuwa huyafahamu.

Sasa leo tumekuja na mada wewe mwanamke inabidi umtambue mwenzawako na kumuelewa sasa hapa tupo na mambo yanayosababisha mwanaume wako awe mdhaifu kitandani sio unapanic tu inabidi umsaidie katika hali yake ya kawaida.

Tunapoongelea mwanaume lazima utaje utendaji kazi wake hasa anapokuwa faragha na mwenzi wake,Watu wamekuwa wakiamini kuwa kitendo cha mwanaume kukosa hamu ya kushiriki na mwenza wake inaweza kutokana na kupungua kwa nguvu za kiume.

Ukitaka mwanaume akose furaha basi ashindwe kabisa mbele ya mwanamke, Jambo hilo waga ni tusi kubwa zaidi ya matusi mengine. Ungana nasi kufahamu tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume kitaalamu ni jambo la kawaida, japo huambatana na baadhi ya sababu za kiafya, kisaikolojia na pengine suala zima la maisha.

 

SABABU ZA MWANAUME KUWA MDHAIFU UKIWA FARAGHA

  1. Upungufu wa homoni

Testesterone kitaalamu hii ni homoni ambayo ipo kwenye maimbile ya mwanaume, kazi yake kubwa ni kuimarisha misuli, kuboresha uzito wa mifupa na kutengeneza mbegu za kiume. Homoni hii kwa kiasi kikubwa huongeza hamu ya tendo, kitendo cha homoni hii kupungua kunaweza kusababisha hamu ya tendo kupungua

  1. Msongo wa mawazo

Mwanaume akiwa na mfadhaiko au msongo wa mawazo, lazima utendaji wake wa mwili huathirike kwasababu msongo wa mawazo husababisha hitilafu kwenye homoni na kusababisha mishipa ya ateri kubana na kuzuia damu wakati wa tendo. Wanaume wengi wanaopita kwenye hali hii na hutafuta dawa za kujitibu na inaelezwa kuwa dawa hizo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hamu ya tendo la ndoa. 

  1. Magonjwa ya muda mrefu

Kitaalamu magonjwa ya muda mrefu kama vile kansa, kisukari na mengine kama hayo yanasababisha maumivu ni vigumu kwa mwanaume kushiriki tendo la ndoa, maana hupunguza kiwango cha kutengeneza mbegu za kiume.

Matumizi ya madawa ya kulevya na pombe kupindukia kwa kiasi kikubwa huchangia tatizo hili lakini pia unywaji wa pombe kupita kiasi na wenyewe huchangia kupungua katika kushiriki tendo hilo.

  1. Kutojiamini na unene uliopitiliza

Ni ngumu kwa mwanaume mwenyewe hajimini ikitokea mwanaume hajiamini humpelekea wasiwasi wa mvurugiko wa homoni zinazomsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Mwanaume mnene kupitiliza anaweza kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa endapo homoni ya testosterone itapungua na pia unene unaweza sababisha ugonjwa wa moyo ambao unaweza kumfanya asishiriki vizuri tendo la ndoa

  1. Umri mkubwa

Kitaalamu mwanaume anapofiakia umri wa miaka 60 mpka 65 homon zake za kutengeneza mbegu za kiume hupungua kabisa na kupelekea hisia za tendo la ndoa kupotea kabisa muda mwingine kuchelewa kufika kwa wakati.






Comments 1


  • Awesome Image
    Ali

    Sorry mnaonaje kama mngeweka tiba ambayo inatakiwa itumike kwa mtu ambae yupo na hilo tatizo

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post