Mambo yanayoharibu battery ya simu yako

Mambo yanayoharibu battery ya simu yako

Hivi unafahamu kuwa kuna mambo mengi ambayo yanachangia sana baterry ya simu yako kutokuwa na uwezo wa kukaa na charji kwa muda mrefu, je unafahamu ni mambo gani hayo? Fuatilia kwa umakini sana dondoo hii.

Leo kwenye smartphone bwana nitakuelekeza mambo ambayo yanasababisha smartphone yako kushindwa kukaa na chaji usishangae sana mambo madogo tu ukiyazingatia mambo yatakua bulbul.

Epuka kuchaji simu yako kila wakati

Kucharji simu yako kila mara ni kosa ambalo hufanywa na watu wengi sana, hapa sasa unakuta mtu anacharji simu yake bila hata kujali kama simu imeisha chaji au la nikwambie tu kwa mujibu wa utafiti battery za simu hupata maisha marefu na kudumu na charji pale inapochajiwa ikiwa na asilimia 10 au 20.

Kuchaji simu huku umeweka kava kwenye simu

Hili nalo tuwe nalo makini sana maana wengi wetu tunanunua simu za gharama hivyo inatulazimu kuweka protector na makava ili kuzilinda lakini baadhi ya makava huchangia uharibifu wa battery zetu bila wenyewe kujua.

Mara nyingi tunavyochaji simu zetu unakuta unachaji huku cover likiwa kwenye simu yako hili ni kosa kubwa na huchangia kuharibu battery ya simu yako.

Kuweka wallpaper zenye rangi nyingi angavu

Hili nalo neno maana wengi wetu tunapenda sana kupendezesha zaidi simu zetu mara nyingi unapokuwa umeweka picha zenye rangi nyingi angavu simu yako hutumia chaji nyingi zaidi kuweza kuonyesha rangi zote hizo kwenye kioo chako.

Kutumia charji ambazo hujaza simu haraka

Hii ipo sana kwenye jamii yetu mara nyingi watu wengi wamekuwa wakidai kuwa wanapenda aina flani ya chaja kwa sababu inacharji battery haraka.

Hili sio sawa na linaweza kuharibu simu yako kwasababu mara nyingi chaji hizi hutoa umeme mkubwa kuliko inavyostahili badala yake angalia simu yako kama ina teknolojia ya Fast charging na kuhakikisha unanunua chaja yenye teknolojia hiyo.

Nikwambie tu kuwa umakini unahitaji sana kwenye matumizi ya smartphone zetu mambo madogo madogo yanaweza kuathiri bila mwenyewe kutambua zingatia hayo itakusaidia kutunza battery ya simu yakooo!!!

Em Tuambie, uliyajua haya?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags