Mambo yanaweza kufanya mwanaume akupende

Mambo yanaweza kufanya mwanaume akupende

Hellow! Watu wangu wa nguvu basi bana ni siku nyingine tena leo katika mahusiano tunakusogezea mada moja matata sana, kama tunavyojua siku zote kuwa Mapenzi ni jambo gumu lakini haiwazuii watu  kuendelea  kupendana Kila dakika inayopita watu hukutana, kuoana, kuanzisha familia, na kuunda ushirikiano wa maisha.

Watu hutumia miaka wakingoja na kutafuta kitu au watu wa kweli na safi, Haijalishi unafanya nini usikate tamaa juu yako mwenyewe katika kutafuta upendo.

Haya ndo mambo unayotakiwa kuyafanya ili mwanaume wako aweze kukupenda Zaidi

  1. Kujiamini

Jambo la kwanza kabisa ni kujiamini na kuweka imani kwa mpenzi wako hatukatai kuna time lazima utamfikiria vibaya kuhusu yeye lakini ili kudumisha mahusiano yako na ndoa yako inabidi ujiamini uko peke yako hata kama hauko peke yako, Kujiamini kila wakati ni nyenzo kuu - usiwe na woga juu ya kuonyesha kujiamini kwa kiwango cha juu.

  1. Jifunze kuskiliza/ kumskiliza mwenza wako

Kila uhusiano wenye afya unategemea mawasiliano na kupata upendo wa kweli utategemea pia Ni lazima uwe na nia ya dhati kwa mtu ambaye ungependa kuwa nae, kama hamjui sasa leo nawajuza kuwa wanaume pia wanamatatizo na wanahitaji kuskilizwa so jitahidi sana kumsikiliza mwenza wako ujue shida zake na mambo yanayo mkabili, tatizo la wanawake wengi wanapenda kulalamika na kupeleka shida zao kwa wanaume zao kuliko kuwaskiliza wenzao.

  1. Jifunze kumsoma mwenza wako/ angalia ndani ya nafsi yake

Wanasema kwamba "macho ni vioo vya nafsi zetu" kwa sababu. Kutazamana kwa macho ni muhimu katika mawasiliano yoyote hasa unapojaribu tu kumjua mtu. Vinywa vyetu vinaweza kusema chochote tunachotaka lakini macho yetu mara chache hudanganya. Mwangalie, soma uso wake, tabasamu, hivi vyote vitakupa ujumbe kuwa anakudanganya au anazungumza ukweli.

  1. Muheshimu mwanaume wako katika kila jambo

Siku zote Mwanaume anataka na kupenda kujisikia kama mwanaume na kuthaminiwa kwa uwezo wake haijalishi ni jambo jema au laah ila jitahidi sana kumuheshimu mana wanadamu hatujakamilika sio kila siku atatenda jambo jema, chakufanya ni kutumia muda zaidi pamoja naye.

  1. Jifunze kumteka mwenza wako

Sisi sote tunapenda kuamini kwamba tuna haiba ya kuvutia, hapa sizungumzii kumteka kama unavyo fikiria wewe nazungumzia kumfanya akupende kumuonesha ni jinsi gani unafuraha ukiwa nae, shiriki katika huzuni yeka, Shiriki mawazo yako na matamanio yako - mwonyeshe ndoto zako kuwa unatamani kufanya jambo gani na jambo gani, hapo utakuwa umemteka kifikra na kugundua kuwa wewe ni mwanamke sahihi kwake.

  1. Kuwa wewe

Nikizungumza kuhusu kuwa wewe kila mtu anaelewa usipritend maisha ishi maisha yako, jitahidi kukubaliana na uwezo aliojaliwa mwenzawako, kuna baadhi ya mabinti wanalalamika wanaachwa mara kwa mara lakini sababu kubwa ni kutamani mahusiano ya mtu mwingine au rafiki yake.

Ukiuwa katika mahusiano inabidi kuonyesha rangi zako halisi! Unashikwa na uwongo kila wakati unapojaribu kuficha kitu. Jaribu Kuwa wewe mwenyewe na kubaki mwaminifu kwa wewe ni nani. Kuwa mtulivu, muwazi, na unyenyekevu ni mambo ya kuvutia zaidi kwa msichana.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags