Mambo ya msingi kuyafanya boom linapoingia

Mambo ya msingi kuyafanya boom linapoingia

Ooooooooh! Haya haya wale wanangu wa vyuoni, kama mnavyojua hakuna siku ya furaha kama siku boom linapoingia, labda kama ulikuwa na madeni mengi na unaona ukilipia boom unabaki hauna kitu, basi hapo kweli unakuwa hauna furaha siku ambayo boom linaingia.

Ila wengi wetu huwa furaha inakuwa kubwa na tunaamini kuwa shida zimeisha na hivyo huo ndio muda wa kuanza kula raha na bila ya kuwa na bajeti tunajikuta hela imeisha mapema hata wiki mbili hazijapita.

Kama wewe ni mmoja wa hawa niliowataja hapa basi fanya mambo haya mara tu boom linapoingia ili kuepuka matumizi mabaya ya pesa hiyo.

Haya ndo mambo 5 ya kuyafanya pale boom linapoingia:

  • Weka kiwango fulani kwenye akiba kabla haujafanya manunuzi yoyote.

Akiba haiozi, uwe na kiwango fulani ambacho unakiweka kwenye akiba labda ambayo utaitumia ukimaliza chuo au siku ukiishiwa kabisa na hela. Unaweza ukafungua hata fixed account kwaajili ya kuweka hela hii au ukaweka kwenye huduma za simu.

  • Weka bajeti ya matumizi yako yatakuwaje ya hiyo pesa.

Hii itakusaidia kulipia matumizi yako kwa ufasaha na wakati. Nashauri kabla hata halijaingia ukisign tu, kaa chini ulipangie bajeti ya matumizi ili likiingia ujue unalitumiaje.

  • Toa hela ya kulipa madeni au mahitaj mbalimbali.

Kwa mnaokaa offsite hata kabla haujawaza kingine, lipia bili zinazohitajika, kwa mnaoweka bili za chakula huu ndio muda mzuri wa kulipia hilo, lipia mahitaji na madeni mapema kabla haujatumia au kujipa moyo pole na kughairisha kulipa.

  • Tenga kiwango kidogo cha pesa cha kutembea nacho mkononi.

Kama tunavyojua siku zote kuna emergency inaweza kutokea muda wowote, so unapopangia bajeti basi weka na kiasi kidogo utakachoweza kutembea nacho mfukoni. Waswahili wenyewe wanasema unaweza angusha nyanya za watu na hauna shillingi kumi mfukoni, watu watakuwa hawakuelewi.

Siku hiyo badilisha hata mlo au jinunulie kitu ambacho ulitamani kukinunua kwa muda mrefu. Najua kuna wengine kama mimi ambao boom lilikuwa linahitajika na familia pia ila hakikisha pia na wewe unapata kulitumia maana unaweza maliza chuo kama vile haukuwa na boom maana hauna kumbukumbu ya pesa uliitumiaje au ulienjoy vipi nayo. Siku moja moja kumwagilia moyo sio mbaya my wangu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post